Header Ads

Jinsi Ya Kuishi Katika Mahusiano Marefu Na Mpenzi Wako


 Kuwa katika relationship ni ngumu na pia ni rahisi. Kuna watu ambao hujaribu kuingia katika relationship lakini baada ya siku mbili tatu unaona wamekosana na mwisho kuachana. Pia utapata wengine wanakuwa katika relationship miaka mitano hata kumi na zaidi.

Hapo unaachwa na maswali yasiyokuwa na majibu ukijiuliza ni mbinu gani inayowafanya wapenzi hao wawili kudumu katika mahusiano marefu kama hayo.

Well, kama wewe umeingia katika mahusiano na unataka yawe marefu basi kuna sheria na masharti ambayo unapaswa kufuata ili kuhakikisha mahusiono yako yatakuwa marefu. Baadhi ya mambo ya kufuata na kuzingatia ni kama yafuatayo:

1. Kuwa na nafasi binafsi. Katika mahusiano, yawe mapya ama ambayo yameshamiri, lazima uwe na nafasi yako binafsi. Hii inatumika kwa yeyote ambaye hayuko single. Kama mnaishi pamoja basi unahitaji kuwa na nafasi ya kuwa kivyako. Hakikisha kuwa unameet na marafiki zako, nenda kafanye mazoezi, soma vitabu ili mradi tu unakuwa na uhuru wa kufanya mambo kivyako.

2. Chagua vitu vya kupigania. Kama mmekuwa mkiishi pamoja na mpenzi wako, kufikia sasa najua kuna mambo mengi ambayo unayajua kumhusu mpenzi wako unayoweza kuyatumia dhidi yake, jambo ambalo si zuri.

So badala ya kugombana kila wakati kuhusu mambo madogo madogo, ni bora kurudi nyuma na kufikiria ni mambo gani muhimu ambayo yanahitaji kupiganiwa.

3. Mazungumzo yaendelee kunawiri. Wengi katika mahusiano huchukulia kuwa wamekuwa katika mahusiano muda mrefu na wapenzi wao hivyo hawaoni umuhimu wowote wa kuwasiliana na wapenzi wao. Unachohitajika nikuendeleza kiwango cha mawasiliano na mpenzi wako muda wote. Usibahatishe hata mara moja.

4. Tokeni deti. Kutoka deti kuna umuhimu kwa kuwa mnapata kukumbana na mambo mapya. Mpenzi wako atafurahia kwa kuwa unaleta misisimiko mipya katika maisha yenu. Hivyo kumtoa mpenzi wako deti kuangalia sinema, mkahawa ama kwenda katika sehemu za kujipumbaza kunafungua maisha mapya kati yenu.

5. Usitarajie chochote. Ukimsapraize mpenzi wako na ua ama zawadi yoyote hupaswi kutarajia chochote kutoka kwake. Kuwa katika mahusiano hakumaanishi kuwa ukitoa unapaswa kunufaika, la. Wewe unapaswa kutoa ili umfurahishe mpenzi wako. Inaonyesha kuwa unamkubali mpenzi wako, na watafurahi katika mahusiano yenu.

6. Wewe si mtu wa kusuluhisha matatizo. Hapa ndipo wengi hukosea. Wakati umekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu, huwa inafikia mahali flani tunayachukulia matatizo ya wapenzi wetu kama ni yetu. Ni kweli kuwa matatizo yao kwa njia moja au nyingine yanaweza kutuathiri, lakini ukweli ni kuwa hupaswi kumsaidia. Mwache apigane na matatizo yake hadi mwisho. Wewe unachotakiwa kufanya ni kumpa sapoti tu. Ukiwa mtu wa kumtatulia matatizo yake basi unapoteza kile cheo cha kuwa mpenzi wake.

7. Gombana naye kijanja. Kugombana na mpenzi wako kwa kawaida huwa ni njia mnayofanya ili kutafuta suluhisho. Lakini wakati unapogombana naye lazima uwe mjanja. Tabia ya kumpigia kelele na kumuita majina machafu hakufai kabisa. Ukiwa mkweli na ukiongea na mpenzi wako vizuri kutatatua matatizo yenu haraka sana.

8. Heshimu mipaka yenu. Kina mtu huwa ana mipaka yake ikija katika mahusiano hivyo hakikisha unaijua mipaka ya mpenzi wako na hupaswi kuivuka. Kama utamtania basi jua kile kiwango ambacho kinahitajika na wala usipitishe.

9. Kuwa na malengo yako. Hili ni muhimu. Uko katika mahusiano lakini pia wakati huo huo wewe ni mtu binafsi. Kama unataka kuwa mtu bora basi ni lazima uwe na malengo yako katika maisha. Kufanya kazi ili utimize ndoto zako kutakufanya kuwa mtu mzuri katika mahusiano.

10. Mpenzi wako atabadilika. Ama labda anaweza asibadilike. Lakini jua na mapema ili isikuwe kama saprize kwako. Watu hubadilika na kuwa wakubwa. Hivyo ni jambo huwezi kuliepuka. Unachohitajika kufanya ni kuhakikisha kuwa unamsaport mpenzi wako wakati wa mabadiliko ya maisha ambayo atayapitia.

11. Mapenzi yatabadilika. Unaweza kukumbuka mara ya kwanza venye mapenzi yalipokuwa yamenoga. Mapenzi hubadilika. Lakini haimaanishi kuwa upendo wenu umepungua, la. Huwa ni hatua ambayo lazima uipitie katika mahusiano. Kuna wakati ambao mapenzi yanashika na wakati ambapo yanapungua pia.

12. Chekeni pamoja. Hili ni jambo muhimu katika mahusiano. Unahitajika kucheka na mpenzi wako. Kucheka pamoja huwa tamu zaidi kuliko tendo la ndoa. Kumbushaneni yale mambo ambayo mmepitia na mcheke pamoja.

13. Muamini mpenzi wako. Kufikia mwisho wa siku hakuna kitu muhimu katika mahusiano marefu kuliko kumuamini mpenzi wako. Kama huwezi kumuamini mpenzi wako basi huwezi kutumia haya mawaidha yetu hapa Nesi Mapenzi vile inavyohitajika. Kama unataka kujenga uaminifu na mpenzi wako basi lazima uwe muwazi, mkweli na mdhaifu mbele zao.

No comments